JINSI KARANGA INAVYOSAIDIA KUIMARISHA AFYA YA MOYO
Karanga NI chakula muhimu Sana katika afya ya mwanadamu. Kiukweli karanga imekuwa ikitumika na WATU wachache kwa sababu ya uhaba wa elimu kuhusu karanga.karanga Ina virutubisho vingi asili vinavyoimarisha mwili wa mwanadamu.
Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya monounsaturated fats’ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease).
Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la ‘Journal of Nutrition’ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.
Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye moyo, karanga pia, zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants) kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!
Ili kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu, unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile peanut butte, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.

Nguvu ya karanga
ReplyDelete